Habari Forums
Would you like to react to this message? Create an account in a few clicks or log in to continue.
Search
 
 

Display results as :
 


Rechercher Advanced Search

Keywords

Jinsi  mwanamke  

Latest topics
» MATOKEO YA AWALI UCHAGUZI MKUU 2015
Tukio lingine la Mtoto Albino Kukatwa Kiganja cha Mkono hili hapa, Mama yake Ajeruhiwa Vibaya EmptySun Oct 25, 2015 7:59 pm by Admin

» Upinzani Tanzania wazindua kampeni
Tukio lingine la Mtoto Albino Kukatwa Kiganja cha Mkono hili hapa, Mama yake Ajeruhiwa Vibaya EmptySat Aug 29, 2015 8:11 pm by Admin

» Joke Of the Day
Tukio lingine la Mtoto Albino Kukatwa Kiganja cha Mkono hili hapa, Mama yake Ajeruhiwa Vibaya EmptySun Jun 07, 2015 12:53 pm by Admin

» Tatizo sugu LA Ajira
Tukio lingine la Mtoto Albino Kukatwa Kiganja cha Mkono hili hapa, Mama yake Ajeruhiwa Vibaya EmptySat Jun 06, 2015 7:29 pm by Admin

» Joke Of the Day
Tukio lingine la Mtoto Albino Kukatwa Kiganja cha Mkono hili hapa, Mama yake Ajeruhiwa Vibaya EmptySat Jun 06, 2015 7:28 pm by Admin

» Joke Of the Day
Tukio lingine la Mtoto Albino Kukatwa Kiganja cha Mkono hili hapa, Mama yake Ajeruhiwa Vibaya EmptySat Jun 06, 2015 7:26 pm by Admin

» * MAFURIKO MAKUBWA YATOKEA MWANZA....
Tukio lingine la Mtoto Albino Kukatwa Kiganja cha Mkono hili hapa, Mama yake Ajeruhiwa Vibaya EmptySat Jun 06, 2015 12:35 pm by Admin

» Lakini ungeweza Kama ungetaka
Tukio lingine la Mtoto Albino Kukatwa Kiganja cha Mkono hili hapa, Mama yake Ajeruhiwa Vibaya EmptyWed Jun 03, 2015 1:03 pm by Admin

» Fun fact teehe
Tukio lingine la Mtoto Albino Kukatwa Kiganja cha Mkono hili hapa, Mama yake Ajeruhiwa Vibaya EmptyWed Jun 03, 2015 8:21 am by Admin

May 2024
MonTueWedThuFriSatSun
  12345
6789101112
13141516171819
20212223242526
2728293031  

Calendar Calendar


Tukio lingine la Mtoto Albino Kukatwa Kiganja cha Mkono hili hapa, Mama yake Ajeruhiwa Vibaya

Go down

Tukio lingine la Mtoto Albino Kukatwa Kiganja cha Mkono hili hapa, Mama yake Ajeruhiwa Vibaya Empty Tukio lingine la Mtoto Albino Kukatwa Kiganja cha Mkono hili hapa, Mama yake Ajeruhiwa Vibaya

Post by Admin Mon Mar 09, 2015 9:18 pm

LICHA ya Serikali, jamii na jumuiya ya kimataifa kukemea ukatili dhidi ya watu wenye ulemavu wa ngozi (albino), bado kuna wanaoendelea kung’ang’ania mila potofu za kuamini kwamba bila ya ushirikina unaohusishwa na matumizi ya viungo vya albino, hawawezi kufanikiwa kimaisha, iwe katika kisiasa au kibiashara.

Hayo yanathibitishwa na kuendelea kuripotiwa kwa matukio ya ukatili dhidi ya albino, ambapo usiku wa kuamkia jana, watu wasiojulikana walimshambulia na kumkata kiganja mtoto mwenye umri wa miaka sita, Baraka Cosmas na kisha kutokomea nacho kusikojulikana.

Tukio hilo lililotokea katika kijiji cha Kipeta Bonde la Ziwa Rukwa wilayani Sumbawanga, ambako mtoto huyo anaishi na wazazi wake, Cosmas Yoram (32) na Prisca Shaaban.

Tukio hilo limethibitishwa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Rukwa , Jacob Mwaruanda.

Alisema tukio hilo ni la saa 8 usiku wa kuamkia Jumapili wakati mtoto huyo akiwa amelala na mama yake. Baba wa mtoto huyo hakuwepo wakati huo.

Akielezea zaidi, Kamanda Mwaruanda alisema usiku huo kikundi cha watu wasiojulikana walivamia nyumba alimolala Baraka na mama yake mzazi, Prisca wakiwa na silaha za jadi, ikiwemo mapanga na fimbo na kuanza kumshambulia kwa kumcharaza viboko Prisca baada ya kukataa kuwapatia mtoto huyo, mwenye ulemavu wa ngozi.

“Baada ya kuingia ndani ya nyumba hiyo walimwamuru mama mzazi wa mtoto Baraka kuwakabidhi mtoto huyo, lakini alikaidi ndipo walipoanza kumshambulia kwa kumpiga kwa fimbo sehemu mbalimbali za mwili wake na kumjeruhi vibaya …

“Waliingia ndani baada ya kuvunja mlango wa nyumba hiyo, ndipo katika patashika hiyo wavamizi hao walimkata mtoto Baraka kiganja cha mkono wake wa kulia na kuondoka nacho kusikojuliakana,” alibainisha.

Aliongeza kuwa wakati hayo yakitokea, baba mzazi wa mtoto huyo inadaiwa alikuwa amelala katika nyumba ya mkewe mdogo kijijini humo.

Kwa mujibu wa Mwaruanda, mtoto huyo amelazwa katika katika Kituo cha Afya cha Kamsamba wilayani Momba mkoani Mbeya kwa matibabu akiwa pamoja na mama yake mzazi.

“Watu watatu ambao majina yao yamehifadhiwa, wanashikiliwa na Jeshi la Polisi mkoani hapa kwa mahojiano na uchunguzi zaidi kuhusu tukio hilo unaendelea ili kuwasaka wahusika na kiungo hicho cha kiganja cha mkono wa mtoto Baraka,” alisisitiza Kamanda.

Admin
Admin

Posts : 54
Join date : 09/03/2015

https://habariforums.forumotion.com

Back to top Go down

Back to top

- Similar topics

 
Permissions in this forum:
You cannot reply to topics in this forum