Habari Forums
Would you like to react to this message? Create an account in a few clicks or log in to continue.
Search
 
 

Display results as :
 


Rechercher Advanced Search

Keywords

Jinsi  mwanamke  

Latest topics
» MATOKEO YA AWALI UCHAGUZI MKUU 2015
BURE KABISA: Van Gaal aponda mechi ya Arsenal Kombe la FA EmptySun Oct 25, 2015 7:59 pm by Admin

» Upinzani Tanzania wazindua kampeni
BURE KABISA: Van Gaal aponda mechi ya Arsenal Kombe la FA EmptySat Aug 29, 2015 8:11 pm by Admin

» Joke Of the Day
BURE KABISA: Van Gaal aponda mechi ya Arsenal Kombe la FA EmptySun Jun 07, 2015 12:53 pm by Admin

» Tatizo sugu LA Ajira
BURE KABISA: Van Gaal aponda mechi ya Arsenal Kombe la FA EmptySat Jun 06, 2015 7:29 pm by Admin

» Joke Of the Day
BURE KABISA: Van Gaal aponda mechi ya Arsenal Kombe la FA EmptySat Jun 06, 2015 7:28 pm by Admin

» Joke Of the Day
BURE KABISA: Van Gaal aponda mechi ya Arsenal Kombe la FA EmptySat Jun 06, 2015 7:26 pm by Admin

» * MAFURIKO MAKUBWA YATOKEA MWANZA....
BURE KABISA: Van Gaal aponda mechi ya Arsenal Kombe la FA EmptySat Jun 06, 2015 12:35 pm by Admin

» Lakini ungeweza Kama ungetaka
BURE KABISA: Van Gaal aponda mechi ya Arsenal Kombe la FA EmptyWed Jun 03, 2015 1:03 pm by Admin

» Fun fact teehe
BURE KABISA: Van Gaal aponda mechi ya Arsenal Kombe la FA EmptyWed Jun 03, 2015 8:21 am by Admin

May 2024
MonTueWedThuFriSatSun
  12345
6789101112
13141516171819
20212223242526
2728293031  

Calendar Calendar


BURE KABISA: Van Gaal aponda mechi ya Arsenal Kombe la FA

Go down

BURE KABISA: Van Gaal aponda mechi ya Arsenal Kombe la FA Empty BURE KABISA: Van Gaal aponda mechi ya Arsenal Kombe la FA

Post by Admin Wed Mar 11, 2015 9:42 am

WAKATI wewe unalisubiri kwa hamu pambano kati ya Manchester United dhidi ya Arsenal baadaye usiku, hali haipo hivyo kwa Kocha wa United, Louis Van Gaal. Yeye anasema ‘FA siyo ishu, tatizo ni Top Four jamani’.

Van Gaal anadai kwamba pambano dhidi ya Arsenal baadaye usiku halimuumizi kichwa, badala yake kinachomuumiza ni jinsi ya kuirudisha Manchester United katika nafasi nne za juu baada ya kupotea msimu uliopita.

“Siku zote nataka tufikie malengo tuliyojiwekea. Lengo kubwa tulilojiwekea ni Top Four. Taji ni kitu kizuri sana. Kama umetwaa FA halafu haupo Ligi ya Mabingwa kipi ni muhimu? Kwa wachezaji ni kitu kizuri, kwa kocha ni vizuri lakini dhumuni letu kubwa ni kumaliza Top Four,” alisisitiza kocha huyo Mdachi.

Van Gaal pia alimuunga mkono Kocha Mfaransa wa Arsenal, Arsene Wenger ambaye amekuwa akisema kumaliza Top Four ni kitu muhimu kuliko taji hilo. Van Gaal amemkubalia.

“Nadhani yuko sahihi. Nadhani siku zote Arsene Wenger anasema vitu sahihi. Nadhani kwa klabu, michuano ya Ulaya ni ya juu zaidi na ndiyo maana anasema hivyo. Kumaliza katika Top Four ni kitu kizuri sana. Kwetu sisi nadhani ni muhimu sana,” aliongeza kocha huyo.

Pamoja na kauli yake hiyo, kocha huyo Mdachi amepania kupanga kikosi chake kizito kwa ajili ya pambano hilo huku wachezaji wawili tu katika kikosi chake, Robin van Persie na Juan Mata wakiwa wamewahi kutwaa taji hilo.

“Kila mechi unayocheza ina madhara kwa mechi inayofuata. Kwa sasa tupo katika mbio za panya katika Ligi Kuu ya England na klabu ambayo itashinda mechi ya FA itajisikia vizuri kwa mechi zinazofuata,” alisema Van Gaal.

Hata hivyo, Van Gaal amedai amekerwa na tabia ya watu kutafsiri vibaya kauli zake, hasa pale walipomkariri kuwa timu yake haina mshambuliaji anayeweza kufunga mabao 20 kwa msimu. Pia akakanusha kuwa ana uhusiano mbovu na kocha wake msaidia, Ryan Giggs ambaye alinuna wakati Man United ilipofunga bao la ushindi dhidi ya Newcastle.

Admin
Admin

Posts : 54
Join date : 09/03/2015

https://habariforums.forumotion.com

Back to top Go down

Back to top


 
Permissions in this forum:
You cannot reply to topics in this forum