Habari Forums
Would you like to react to this message? Create an account in a few clicks or log in to continue.
Search
 
 

Display results as :
 


Rechercher Advanced Search

Keywords

Jinsi  mwanamke  

Latest topics
» MATOKEO YA AWALI UCHAGUZI MKUU 2015
Wabunge wa Kenya wanapitisha sheria kinyume na katiba ya nchi  EmptySun Oct 25, 2015 7:59 pm by Admin

» Upinzani Tanzania wazindua kampeni
Wabunge wa Kenya wanapitisha sheria kinyume na katiba ya nchi  EmptySat Aug 29, 2015 8:11 pm by Admin

» Joke Of the Day
Wabunge wa Kenya wanapitisha sheria kinyume na katiba ya nchi  EmptySun Jun 07, 2015 12:53 pm by Admin

» Tatizo sugu LA Ajira
Wabunge wa Kenya wanapitisha sheria kinyume na katiba ya nchi  EmptySat Jun 06, 2015 7:29 pm by Admin

» Joke Of the Day
Wabunge wa Kenya wanapitisha sheria kinyume na katiba ya nchi  EmptySat Jun 06, 2015 7:28 pm by Admin

» Joke Of the Day
Wabunge wa Kenya wanapitisha sheria kinyume na katiba ya nchi  EmptySat Jun 06, 2015 7:26 pm by Admin

» * MAFURIKO MAKUBWA YATOKEA MWANZA....
Wabunge wa Kenya wanapitisha sheria kinyume na katiba ya nchi  EmptySat Jun 06, 2015 12:35 pm by Admin

» Lakini ungeweza Kama ungetaka
Wabunge wa Kenya wanapitisha sheria kinyume na katiba ya nchi  EmptyWed Jun 03, 2015 1:03 pm by Admin

» Fun fact teehe
Wabunge wa Kenya wanapitisha sheria kinyume na katiba ya nchi  EmptyWed Jun 03, 2015 8:21 am by Admin

May 2024
MonTueWedThuFriSatSun
  12345
6789101112
13141516171819
20212223242526
2728293031  

Calendar Calendar


Wabunge wa Kenya wanapitisha sheria kinyume na katiba ya nchi

Go down

Wabunge wa Kenya wanapitisha sheria kinyume na katiba ya nchi  Empty Wabunge wa Kenya wanapitisha sheria kinyume na katiba ya nchi

Post by Admin Wed Mar 11, 2015 9:03 am

TAREHE 23 Februari mwaka huu mahakama kuu ya Kenya ilibatilisha vifungu vinane vya sheria mpya ya ugaidi iliyopitishwa na bunge la nchi hiyo, ikisema vifungu hivyo vimekiuka katiba ya nchi.
Sheria hii iliibua malumbano makali tangu Novemba mwaka jana. Serikali imekua ikiitetea kwa kudai kuwa inailinda nchi kutokana na tishio la wapiganaji wa Al-Shebab kutoka Somalia. Rais Uhuru Kenyatta alisema “inawalinda raia”.
Kwa upande wa pili vyama vya upinzani na wanaharakati wa haki za binadamu wamekuwa wakisema sheria hiyo inakiuka misingi ya haki za binadamu. Wakili wa upinzani James Orengo aliiambia mahakama kuwa sheria hiyo ilikuwa inahujumu haki za kiraia.
Miongoni mwa ibara zilizozuiliwa na mahakama ni ile ambayo inatoa adhabu ya miaka mitatu jela na faini ya dola 55,000 kwa mtu anayechapisha makala au hata kutafuta habari ambazo “zinaingiliana na uchunguzi au operesheni ya kupambana na ugaidi”. Tafsiri ya kifungu hiki inaachiwa dola.
Ibara nyingine iliyozuiliwa ni ile ambayo iliipa polisi uwezo wa kufanya udukuzi wa maongezi ya simu au mawasiliano binafsi. Na ya tatu ni ile iliyoweka kikomo cha idadi ya wakimbizi 150,000 nchini, wakati wakimbizi wa Somalia nchini Kenya kwa hivi sasa ni 600,000. Maana yake wakimbizi 450,000 watimuliwe ingawa wamesajiliwa rasmi.
Upinzani ndio uliowasilisha mahakamani barua ya kupinga sheria hiyo. Wakati huohuo, upinzani na wanaharakati wa haki za binadamu wamekua wakilaani sheria hiyo kwa kusema inakiuka haki za binadamu na kuiweka nchi chini ya utawala wa kipolisi kama ilivyokuwa enzi za Moi.
Akisoma uamuzi wa mahakama, Jaji George Odunga alisema sheria ya usalama wa nchi haiwezi ikatungwa kwa njia ambayo inaminya uhuru wa raia. “Hatuwezi kukandamiza uhuru na haki za kimsingi za kiraia kwa kisingizio kuwa tunapambana na ugaidi. Haya yanapaswa yafanywe kwa kutumia sheria sio nje ya sheria”.
Kwa upande wake, Jaji Isaac Lenaol alisema “Tunahitaji kupambanua baina ya kupiga vita ugaidi na kulinda haki za binadamu”.
Jaji Odunga akawasilisha uamuzi wa mahakama kwa Jaji Mkuu Willy Mutunga ambaye anatarajiwa kuteua jopo la majaji watatu ili kuzidi kuzingatia kesi hii iliyofunguliwa na muungano wa vyama vya upinzani (Coalition of Reforms and Democracy).
Kiongozi wa upinzani Raila Odinga alisema uamuzi wa mahakama “utasaidia sana kuhakikisha kuwa katiba ya nchi inaheshimiwa na haki za kiraia zinalindwa.”
Lakini wanaharakati wengi wamesema mahakama ilipaswa kutupilia mbali sheria nzima. Huu ni msimamo wa tume huru ya haki za binadamu (National Commission on Human Rights).
Serikali imesema inafikiria kukata rufaa ili kufuta uamuzi wa mahakama na kuirejesha sheria kama iliyopitishwa na bunge. Msemaji wa Ikulu, Manoah Esipisu alisema serikali “itaendelea kupambana na makundi ya ugaidi na uhalifu, na itatumia uwezo wake wote ili kuhakikisha kuwa raia wake wanalindwa”.
Muswada wa sheria hii uliwasilishwa bungeni baada ya mfululizo mpya wa mashambulizi ya kikundi cha Kisomali cha Al-Shabab mwishoni mwa Novemba na mwanzoni mwa Desemba mwaka jana. Haya yalifanyika kaskazini mashariki mwa Kenya, katika mkoa wa Mandera na yakasababisha vifo vya watu wengi.
Kabla ya hapo watu 67 waliuawa mnamo Septemba 2013 katika jengo la biashara la Westgate (Nairobi). Ndipo serikali ikaamua “kupambana na ugaidi kwa nguvu zake zote”. Al Shabab ilisema oparesheni hizo zimetokana na uamuzi wa serikali ya Kenya kupeleka maelfu ya wanajeshi wake huko Somalia mwaka 2011. Sheria hii mpya yaelekea ndivyo serikali inavyotunisha misuli yake dhidi ya Al Shabab.
Ni sheria iliyotayarishwa kwa haraka na kuwasilishwa bungeni. Inakiuka haki za kiraia zilizolindwa na katiba ya nchi na hata sheria za kimataifa kuhusu haki za binadamu. Sio tu ilibuni makosa yasiyokuwepo bali pia zinaambatana na adhabu kali
Sheria hii ilibadilisha sheria iliyokuwepo ya usalama wa taifa kwa kumpa afisa usalama uwezo wa kumkamata raia, kumpekua na hata kushika mali zake bila kufuata utaratibu uliowekwa kisheria. Ni pamoja na kusoma barua zake na mawasilianao yake binafsi. Yote haya ni baada ya kushukiwa tu na mwanausalama ambaye hatakiwi kuthibitisha.
Inatukumbusha miaka ya 90 wakati maofisa usalama walipowashika, kuwatesa na kuwafunga wanaharakati kwa muda wa miaka kadha bila ya kuwafikisha mahakamani. Sasa uwezo huo unataka kurudishwa kwa mlango wa nyuma.
Sheria iliyokuwepo inampa mwanausalama uwezo wa kumfunga raia kwa muda usiozidi saa 24. Sasa sheria mpya itampa uwezo wa kumfunga raia siku 90. Na mfungwa hapewi sababu wala ushahidi.
Mtu anayekutwa na silaha kama bunduki atachukuliwa kuwa ni gaidi, naye atawajibika kuthibitisha kuwa yeye si gaidi, badala ya kazi hiyo kufanywa na anayemkamata. Na adhabu yake ni kifungo kinachofikia miaka 20.
Aidha, chini ya sheria hii itamuwia vigumu raia kukosoa au kufichua makosa yanayofanywa na wanausalama au polisi. Mtu ataweza kufungwa hadi miaka 14 iwapo anatamka au anaandika maneno ambayo “yanafikiriwa” kuwa yanawezesha kuhamasisha au kutetea ugaidi.
Maneno hayo ni katika vyombo vya habari au hata katika mtandao wa jamii (social media) kama face book au blogu. Mtu ataweza kufungwa miaka 30 iwapo “atafikiriwa” kuwa anatetea au anaeneza siasa kali. Atafikiriwa na nani? Kwanini kosa la jinai litegemee fikra tu?
Sheria hii pia itakandamiza haki ya kujumuika na kukutana. Maana yake serikali inaweza kuamua kuzuia mkutano kufanyika. Hiyo siyo tena haki ya kiraia kama ilivyo katika katiba.
Kwa wale wanaofikiria kuwa katiba yatosha kuhakikisha haki inatendeka, ni vizuri wakazingatia mfano huu wa Kenya ambayo ina katiba safi iliyokubaliwa na wananchi.
Kwani chini ya sheria hii serikali imepewa uwezo kamili wa kumkamata mshukiwa wa ugaidi na kumfunga kwa muda wa mwaka mmoja bila ya kumfungulia mashtaka. Kifungu hiki kimeachwa na mahakama. Hata hivyo mahakama imefuta kifungu kinachotoa uwezo wa kumfunga kwa muda wa miaka mitatu mwandishi iwapo ataandika makala itakayoingiliana na uchunguzi dhidi ya ugaidi.
Mahakama pia imefuta kikomo cha idadi ya wakimbizi 150,000 kwa sababu ingesababisha kufukuzwa kwa maelfu ya wakimbizi kutoka Somalia, Sudan Kusini, Sudan na kwengineko wanaoishi kihalali nchini Kenya. Hii ingekuwa kinyume na sheria ya kimataifa iliyoridhiwa na Kenya.
Ni vizuri tukaangalia jinsi sheria hii ilivyopitishwa na bunge kabla ya kukataliwa na mahakama kuu.Tarehe 11 Disemba mwaka jana kamati ya bunge ya usalama wa taifa iliwasilisha bungeni mswada wa sheria hii iliyolenga kubadilisha sheria 22 zinazohusu usalama (Security Laws Amendment Bill, 2014).
Sheria kama hii ilipaswa ijadiliwe na raia, kitu ambacho hakijafanyika. Pia katiba inasema sheria kama hii inayoingilia haki za kiraia ni lazima kwanza ipigiwe kura ya maoni, kitu ambacho pia hakikufanyika. Badala yake sheria ilipitishwa kwa haraka.
Mswada huu uliibua mjadala mkali, hata waheshimiwa wabunge wakatwangana ngumi. Wengine wakachanachana mswada na kumtupia spika. Seneta Johnston Muthama kutoka chama cha upinzani alikuwa msikilizaji. Naye akapigwa na kuchaniwa nguo zake. Yote haya yalikuwa yanaonekana nchini kote kupitia luninga. Ikabidi mjadala uahirishwe.
Rais Kenyatta aliwahimiza wabunge waupitishe mswada bila kuchelewa, akidai kuwa utaimarisha usalama wa taifa kwa kupambana na kikundi cha Al Shabab kutoka Somalia.
Desemba 22 mswada ukapitishwa na ukawa sheria baada ya kusainiwa na Kenyatta, ingawa wengi walimsihi asisaini.
Wapinzani wakaamua kufuata mkondo wa sheria kwa kufungua kesi mahakamani.
Kwa kupitisha sheria hii, Kenya imejiunga na nchi kadha ambazo nazo zimetunga kwa haraka sheria zinazotia kabari haki za kiraia. Nchini Pakistan sheria imepitishwa mwaka huu ikianzisha mahakama ya kijeshi kuwahukumu raia wanaotuhumiwa kwa makosa ya kigaidi.
Uingereza pia iliunda sheria kama hii Novemba mwaka jana ili ‘kupambana na ugaidi’. Na Oktoba mwaka jana serikali ya Canada ilitangaza nia ya kuimarisha sheria zilizokuwapo kuhusu ugaidi, kwa kuvipa nguvu zaidi vyombo vya dola.
Marekani nayo ndiyo inaongoza kwa sheria kama hizi. Raia Edward Snowdon amelazimika kuikimbia nchi yake baada ya kufichua ukweli kuhusu jinsi dola inavyohalifu haki za kiraia. Watu wamefungwa miaka nenda miaka rudi katika gereza la Guantanamo bila ya kufikishwa mahakamani.
Halafu hawa eti wanatufundisha demokrasia na utawala bora. Nchi tisa za Magharibi eti ziliwasihi wabunge wa Kenya waheshimu haki za binadamu walipokuwa wakijadili sheria hii mpya. Ni pamoja na Uingereza na Marekani.

Admin
Admin

Posts : 54
Join date : 09/03/2015

https://habariforums.forumotion.com

Back to top Go down

Back to top


 
Permissions in this forum:
You cannot reply to topics in this forum